RonaldoLionelMessi

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Sunday, 30 September 2012

Spurs Yawachapa Kipigo Red Devils

Posted on 09:54 by Unknown
Clint Dempsey jana aliwathibitishia ushindi Tottenham kwa mara ya kwanza wakiwa Old Trafford tangu  December 1989 baada ya kuwapa kipigo mashetani hao wekundu (Man United) na kuwafanya kupoteza mchezo wa pili tangu kuanza kwa ligi hiyo ya Uingereza. 

Huyu ndiye Clint Dempsey akishangilia goli

Wakiwa wanaongoza 2-0 hadi half-time, Spurs walikianza kipindi cha pili kwa kuruhusu goli toka kwa Man United lililofungwa na Luis Nani aliyepokea krosi toka kwa Wayne Rooney ambao waliingia kipindi cha pili kama simba aliyejeruhiwa, lakini muda mfupi tu baada ya kuruhusu goli hilo walipiga tena goli la tatu na kuwafanya vijana wa Man United wachanganyikiwe. Lakini Man United walijitahidi kucheza bila kuonesha kama wamechanganyikiwa na kuelekeza mashambulizi makali langoni mwa Spurs huku wakicheza kandanda safi lililowafanya Spurs kupaki gari kuanzia katikati ya uwanja hadi ndani ya eneo lao la 18, huku Rafael, Wayne Rooney, Evra na hata Rio Ferdinand wakipeleka krosi za kila mara langoni mwa wapinzani wao wakijaribi kutafuta kusawazisha na hata kupata goli la ushindi. Lakini alikuwa ni Shinji Kagawa aliyewapatia Man United goli la pili na la mwisho na kuufanya mchezo kwisha kwa Spurs kuibuka kwa ushindi wa 3-2.

Spurs wakiwa bado hawajapoteza mchezo tangu kufunguliwa kwa ligi hiyo, wanajipatia umaarufu na kujiamini sana chini ya kocha wao Andre Villas-Boas, aliyekuwa kocha wa zamani wa Porto. 

Kuumia kwa Nemanja Vidic kulileta pengo kubwa sana kwa upande wa Man United na kusababisha katikati kuwe na kichochoro ambacho kiliwapatia Spurs urahisi wa kufunga magoli  yao. Pamoja na wachezaji wakongwe Ryan Giggs na Paul Scholes, bado kullikuwa na udhaifu mkubwa kwani Spurs walionekana wenye mbio na nguvu wakiwa na maumbo makubwa zaidi ya Man United. 

Giggs na  Scholes wanashindwa siku hizi kuonesha ule umaarufu wao wa kutawala kiungo na ile tabia ya Giggs kupiga krosi zinazowarahisishia wafungaji kupata magoli mazuri. Kwani walionekana kuzidiwa sana na wachezaji wenye kasi na nguvu nyika Gareth Bale na Moussa Dembele, na kufanya kuonekana kama vile chaguo la Ferguson ni ajali iliyokuwa inasubiriwa kutokea. 

Pamoja na kwamba hakukuwa na wa kumlaumu kati yao kwa goli la Vertonghen kwenye dakika ya 2 tu ya mchezo, lakini ilioneka wazi aliachiwa nafasi ya wazi ya kukimbia kuanzia katikati ya dimba kabla ya kufunga goli. 

Vertonghen, aliyetokea Ajax, aliwapita Nani na Rio Ferdinand wakati alipokimbia kwa mita 35 na shuti lake kumgonga beki wa Man United John Evans kabla halitinga wavuni.

Chelsea wameendelea kubakia kileleni baada ya Juan Mata kuifanya iibuke kwa ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Arsenal. Wapo pointi 3 mbele ya Everon ambao nao waliendelea na ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton. 

Mabingwa watetezi wa Premier League Manchester City wakitokea nyuma walishinda 2-1 dhidi  ya Fulham, wakimuingiza Edin Dzeko aliyewapatia goli la ushindi dakika 3 kabla ya mtanange kuisha.

 

Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • If You Missed Some Games of The AFCON From S.Africa. Here Are Actions in Pictures For You.
  • Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata na Wenzao Waliowasambaratisha Morocco
    Unaweza kuielezeaje mechi hii ya Stars v Morocco?
  • Liverpool Waliompa Kipigo Norwich Hawa Hapa
      Huku Suarez akipiga hat-trick
  • Who has the best squad for title race - United, City, or Chelsea?
    Who has the best squad for title race - United, City, or Chelsea?
  • Ndugu, Soma Hiki Kioja cha Soka Huko Nigeria!
    T imu nne za mpira wa miguu zimesimamishwa kucheza soka nchini Nigeria baada ya mechi zao kuleta matokeo ya utatanishi kwa mechi hizo kumali...
  • Aston Villa vs Newcastle United: Same boat, different engine. Via HITC SPORT
    Alan Pardew's side head to Villa Park just one point ahead of the home team in the league, but differing transfer windows will likely ...
  • Manchester United Transfer Rumours: Cristiano Ronaldo Deal Reportedly Close | Bleacher Report
    Manchester United Transfer Rumours: Cristiano Ronaldo Deal Reportedly Close | Bleacher Report
  • Hatimaye Lulu Aliona Jua.
    Yule msanii maarufu sana hapa nchini kwenye tasnia ya filamu za bongo maarufu kama "Bongo Movie" Elizabeth maarufu kama "Lulu...
  • Pictures: Mario Balotelli's car gets pissed on and greased with bum sweat by Man United fans | 101GG Football news
    Pictures: Mario Balotelli's car gets pissed on and greased with bum sweat by Man United fans | 101GG Football news
  • Celtic Yawafanyia Kweli Barcelona
      Timu ya Celtic jana  usiku ilionesha kwamba Barcelona si chohcote kwao baada ya kuwatungua mara mbili kwa magoli yaliyowekwa kimiani na Wa...

Blog Archive

  • ►  2013 (172)
    • ►  August (33)
    • ►  July (29)
    • ►  June (40)
    • ►  May (10)
    • ►  April (9)
    • ►  March (28)
    • ►  February (6)
    • ►  January (17)
  • ▼  2012 (128)
    • ►  December (47)
    • ►  November (18)
    • ►  October (48)
    • ▼  September (15)
      • Liverpool Waliompa Kipigo Norwich Hawa Hapa
      • Picha 4 za Jinsi Man United Walivyokamatwa na Spur...
      • Spurs Yawachapa Kipigo Red Devils
      • Manchester United and Tottenham Hotspurs Clash His...
      • Eto'o Atangaza Kurudi Timu ya Taifa
      • Roberto Di Matteo na Mechi ya Leo Dhidi ya Arsenal
      • Arsenal Dhidi ya Chelsea Kesho
      • Why Cristiano Ronaldo Is the Tiger Woods of World ...
      • John Terry – Guilty and Not Guilty…What’s the diff...
      • Do You Know What Was Darren Fletcher's Dream?
      • John Terry is GUILTY in Racism Scandal
      • Wigan boss charged over post match comments agains...
      • Mourinho Could Manage Into His 70s: Originally Rep...
      • Rihanna with Her New Single "Diamonds"
      • 50 Cent Investigation
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile